MASIKINI SUAREZ! ADHABU YA KUFUNGIWA MIAKA MIWILI YAMSUBIRI … ushiriki wake wa mechi zilizosalia za World Cup mashakani



MASIKINI SUAREZ! ADHABU YA KUFUNGIWA MIAKA MIWILI YAMSUBIRI … ushiriki wake wa mechi zilizosalia za World Cup mashakani

Security: Uruguay's team hotel in Natal has been                  surrounded by armed guards in response to the incident

MSHAMBULIAJI matata wa timu ya soka ya Uruguay Luis Suarez anakabiliwa na adhabu ya kufungiwa kwa mrefu itakayomlazimu kukosa mechi zote za michuano ya kombe la dunia iwapo atapatikana na hatia ya kumng'ata mchezaji wa Italy Giorgio Chiellini.

Shirikisho la soka duniani FIFA limeanzisha harakati za kumuadhibu mcheza huyo kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Italy siku ya Jumanne.

Chiellini amedai kwamba Suarez alimng'ata bega lake licha ya Suarez kudai kuwa ni mchazaji huyo aliyemchezea vibaya.

Suarez mwenye umri wa miaka 27 huenda akapigwa marufuku kucheza mechi 24 ama miaka miwili.

Refa aliyesimamia mechi hiyo kutoka Mexico Marco Rodriguez hakuchukua hatua yoyote kufuatia kisa hicho,lakini FIFA bado inaweza kumuadhibu Suarez.

Aliyekuwa mchezaji wa kiungo wa zamani wa Liverpool Jan Molby anatarajia kwamba Suarez atapigwa marufuku kwa mechi zote za kombe hilo zilizosalia.

Raia huyo wa Denmark ameliambia gazeti la Liverpool la Echo kwamba '' nina hakika FIFA itachukua swala hilo la Suarez kama mfano kwa wengine''.

''Ni dhahiri kwamba matumaini yake ya kushiriki katika michuano ya kombe la dunia iliosalia yamekwisha na ninataraji kwamba FIFA itampatia adhabu ya muda mrefu''.

Hata hivyo Suarez amesema kilichotokea ni kwamba aligongana na bega la mchezaji huyo wa Italia na kujitetea kuwa katika soko vitu hivyo hutokea.



Comments