Wachezaji wa Yanga sasa                    kuanza mazoezi chini ya Maximo
          KOCHA mpya wa Yanga sc,                  Mbrazil Marcio Maximo ameanza kazi leo kwa kufanya                  mazungumzo na baadhi ya wachezaji wa klabu hiyo .
          Mkutano huo umefanyika makao                  makuu ya klabu ya Yanga, makutano ya Twiga na Jangwani,                  Kariakoo, jijini Dar es salaam.
          Maximo alipata nafasi ya                  kuwaeleza mipango yake ya kazi na kuwataka wachezaji                  waelewe umuhimu wao katika kujenga mafanikio ya Yanga.
          Kocha huyo aliyewahi kufanya                  kazi nchini kwa kuifundisha timu ya Taifa ya Tanzania,                  Taifa stars,  baada ya kukutana na wachezaji leo hii,                  sasa yuko tayari kuanza mazoezi ya kujiwinda na msimu                  mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara unaotarajia kuanza                  mwezi agosti mwaka huu.
          Pia Yanga itashiriki michuano                  ya kombe la kagame na kombe la shirikisho barani Afrika                  baada ya kumaliza katika nafasi ya pili msimu uliopita.
          Maximo katika programu yake                  atakuwa na wachezaji ambao hawako kwenye vikosi vya timu                  za taifa kujiandaa na michezo ya kuwania nafasi ya                  kupangwa hatua ya makundi ili kusaka tiketi ya fainali                  za AFCON mwakani nchini Morocco.
          Baadhi ya wachezaji wa Yanga                  akiwemo nahodha, Nadir Haroub `Cannavaro`, kipa                  Deogratius Munish `Dida`, Kelvin Yondani, Oscar Joshua                  na wengineo wapo na kikosi cha Taifa stars katika kambi                  ya wiki mbili mjini Gabarone, nchini Botswana.
          Wakati Yanga wakifurahia na                  ujio wa Maximo, kwa upande wa Simba wamekamilisha                  uchaguzi wao hapo jana.
          Evans Elieza Aveva alishinda                  kwa kishindo dhidi ya Andrew Peter Tupa na kuwa rais wa                  kwanza wa Simba .
          Naye Goefrey Nyange `Kaburu`                  aliibuka kidedea katika kinyang`anyiro cha umakamu wa                  rais wa klabu hiyo.
          Wajumbe walioshinda na kuingia                  katika kamati ya utendaji ya Simba sc ni Idd Kajuna,                  Coliins Friesh, Ally Suru na Saild Tully. Kwa upande wa                  mwanamke ni Jasmin.
        
Comments
Post a Comment