MANCHESTER United imekaa mkao wa kula kumalizana na Arsenal juu ya beki wa kati Thomas Vermaelen.
Beki huyo amekuwa hana namba katika kikosi cha kwanza cha Arsenal na sasa bosi mpya wa United Louis Van Gal anataka kumpa maisha mapya nyota huyo wa Ubelgiji.
Huku tayari ikiwa na mapengo ya Nemanja Vidic na Rio Ferdinand, hatua ya kuimarisha safu ya ulinzi ni jambo la kufa na kupona Old Trafford.
Vermaelen amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake wa kuitumikia Arsenal hivyo suala la uhamisho wake linaonekana ni lenye manufaa kwa pande zote tatu (Man United, Arsenal na Vermaelen).
Inaaminika United italipa kati ya pauni milioni 10 na 11 katika kipindi hiki wanachojaribu kusajili beki wa pili baada ya kumnasa Luke Shaw kwa pauni milioni 34 kutoka Southampton.
Comments
Post a Comment