BAADA ya Manchester United kukamilisha usajili wa kiungo Ander Herrera kwa pauni milioni 29 kutoka Athletic Bilbao, sasa inatarajiwa kumalizana na Luke Shaw masaa machache yajayo.
Luke Shaw beki wa kushoto wa Southampton mwenye umri wa miaka 18 anatarajiwa kupima vipimo vya afya Ijumaa kabla ya kukamilisha usajili wa pauni milioni 34.
Alhamisi jioni, Luke Shaw aliwasili kwenye uwanja wa mazoezi wa United na kutarajiwa kulala jijini Manchester ambapo Ijumaa baada ya vipimo atapelekwa Old Trafford kwaajili ya picha za promosheni.
Huo utakuwa usajiliwa pili kwa Manchester United ndani ya wiki moja.
Herrera amesaini mkataba wa miaka minne utakaOmpatia mshahara wa pauni 70,000 kwa wiki.
Comments
Post a Comment