Mshambuliaji wa Liverpool anaweza kwenda Barcelona kwa dau la puandi milioni 80.
Siku za furaha: : Suarez akishangilia kushinda kiatu cha dhahabu pamoja na mtoto wake Delfina na mke wake Sofia
Liverpool wameanza mbio za kumuwania mchezaji wa Benfica, Lazar Markovic.
Mserbia, Markovic ni moja ya wachezaji bora wenye umri mdogo katika soka la Ulaya na bei yake ni paundi milioni 20.
Japokuwa Liverpool walikuwa wanaweka ngumu kwa dau hilo, lakini baada ya kupokea taarifa za FIFA kuhusu kumfungia Suarez wamelazimika kukubali na kumruhusu Muurguay huyo kuondoka klabuni hapo.
Licha ya kufungiwa, Liverool wanaamini Barcelona inaweza kulipa paundi milioni 80 na tayari mmiliki mkuu wa klabu hiyo John W Henry anaonekana kutokuwa tayari kumuuza kwa bei rahisi.
Mwanasheria wa Suarez Alejandro Balbi alikuwa Barcelona kujadili hatima ya mteja wake, wakati kocha mpya wa Barca Luis Enrique alisema hakuna tatizo lolote juu ya kumsajili nyota huyo mwenye miaka 27.
Alimfananisha Suarez na mshambuliaji gwiji wa Barca Hristo Stoichkov na alisema : 'Stoichkov kiukweli aliwahi kufanya madhambi makubwa dhidi ya mwamuzi, lakini aliendelea kufirika kuwa mcheza mkubwa".
Kama Liverpool watamuuza Suarez kwa paundi milioni 80, hiyo itakuwa biashara nzuri kwa Brendan Rodgers ambapo atatumia mkwanja huo kuimarisha kikosi chake.
Comments
Post a Comment