LIVERPOOL inakamilisha taratibu za mwisho kabisa kumsajili kiungo wa Southampton Adam Lallana mara baada ya timu hizo mbili kukubaliana ada ya pauni milioni 25 kwaajili ya uhamisho huo.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa England alionyesha mapema kuwa moyo wake uko Merseyside mara tu baada msimu uliopita kufika ukingoni ambapo sasa njozi yake hiyo inahesabu masaa tu kabla ya kugeuka kuwa kweli.
Lallana ameelekea makao makuu ya mazoezi ya Liverpool (Melwood) kwaajili ya vipimo vya afya kabla ya kutangazwa rasmi kujiunga na kikosi hicho kinachonolewa na Brendan Rodgers.
Comments
Post a Comment