Muda mchache baada ya timu              yake kuondolewa rasmi kwenye michuano ya kombe la dunia kwa              kushindwa kufanya vyema katika mechi za makundi kwa mara ya              pili mfululizo katika kombe la dunia, kocha Cesar Prandelli              amefanya maamuzi magumu.Italia iliondolewa baada ya kufungwa              kwa goli 1-0 na Uruguay katika mechi ya mwisho ya              makundi.Baada ya mchezo Prandelli akiwa kwenye mkutano wa              waandishi wa habari alitangaza kujiuzulu kuifundisha timu              hiyo."Nilichagua mfumo fulani wa ukufunzi na ndio sababu              ninajiuzulu, kwa sababu haukufanya kazi," alisema.
        Aliongezea: "Kuna jambo              ambalo limebadilika tangu nilipotia saini mkataba mpya.              Sijui kwanini lakini sina haja ya kutafuta sababu ."
        Kocha huyo aliingia              mkataba mpya na Italy Mei mwaka huu ambao ungemfanya              aendelee kuifundisha Italy hadi baada ya mashindano ya              kuwania ubingwa wa Euro ya mwaka wa 2016.
        Prandeli amechukua hatua              hii baada ya kujiuzulu kwaa rais wa shirikisho la kandanda              la Italia Giancarlo Abete.
        "Nilizungumza na rais wa              shirikisho na naibu wa rais Demetrio Albertini na nikawapa              barua ya kujiuzulu kwangu. Ni jambo lisilobadilika,"
        
Comments
Post a Comment