KILIO AFRIKA: SARE TU ILIHITAJIKA LAKINI BAO LA DAKIKA 90 LAING’OA IVORY COAST KOMBE LA DUNIA …Colombia nayo yaifanyia kitu mbaya Japan


KILIO AFRIKA: SARE TU ILIHITAJIKA LAKINI BAO LA DAKIKA 90 LAING'OA IVORY COAST KOMBE LA DUNIA …Colombia nayo yaifanyia kitu mbaya Japan

Last-ditch: Greece defender Konstantinos Manolas                    dispossesses Salomon Kalou

IVORY COAST imeleta msiba mkuwa kwa mashabiki wa soka wa bara la Afrika baada ya kufungwa 2-1 na Ugiriki katika mchezo ambao sare tu ingetosha kuwavusha wawakilishi hao wa Afrika.

Huku mchezo ukielekea kwisha kwa matokeo ya 1-1, Ugiriki wakapata penalti katika dakika ya mwisho ya mchezo (90+2) na kuzaa bao la pili kupitia kwa Georgios Samaras.

Bao hilo likafuta matumaini ya Ivory Coast kutinga 16 bora kwa mara ya kwanza katika historia yao ya ushiriki wa kombe la dunia mara tatu.

Ugiriki walipata bao lao la kwanza kupitia kwa Andreas Samaris dakika chache kabla ya mapumziko kabla ya Ivory Cost kusawazisha kwa bao tamu la Wilfried Bony dakika ya 74.

Opener: Andreas Samaris fires Greece into the lead                  against the Ivory Coast in Group C on Tuesday night

Bao la kwanza la Ugiriki

Get in! Greece players congratulate Samaris after the                midfielder put his side in front against the Ivory Coast

 

Furaha ya bao la kuongoza

Equaliser: Ivory Coast striker Wilfried Bony shoots                  and scores to equalise for his side against Greece

Ivory Coast wanasawazisha

Team effort: Ivory Coast players celebrate Bony's                equaliser and congratulate the striker

Furaha ya bao la kusawazisha

Ivory Coast itabidi wajilaumu wenyewe kwa kukaribisha mashambulizi mengi ukingoni mwa mchezo huku pia kiungo wake Yaya Toure akipoteza nafasi ya wazi ya kufunga bao la pili.

Kwa matokeo hayo, Colombia na Ugiriki ndio zinazotinga hatua ya 16 bora kutoka kundi C.

Colombia iliyotwaa nafasi ya kwanza, imefiksha pointi tisa baada ya kuinyuka Japan 4-1.



Comments