Kilichojiri kwenye mechi za Ivory Coast vs Ugiriki na Japan vs Colombia


Kilichojiri kwenye mechi za Ivory Coast vs Ugiriki na Japan vs Colombia
20140625-073450-27290496.jpg
Matumaini ya bara la Afrika kuingiza timu kwenye hatua ya 16 bora ya michuano ya kombe la dunia yameanza kupotea.Wakicheza mchezo wao muhimu na wa mwisho, Ivory Coast ilikubali kipigo kutoka kwa Ugiriki katika mchezo ulioisha kwa kufungwa 2-1.Kufuatia ushindi huo Ugiriki imeungana na Colombia kwenda hatua ya pili kutoka kwenye kundi hilo.Ugiriki ilikuwa ya kwanza kufunga kupitia bao la kwanza la Georgios Samaras kunako dakika ya 42 ya kipindi cha kwanza baada ya mlinzi wa Ivory Coast Cheick Tiote kufanya makosa ya kipuuzi.

Ivory Coast hata hivyo ilifunga bao la kusawazisha kupitia Wilfried Bony aliyetumia vyema pasi safi kutoka kwa Gervinho.
Ugiriki walipata goli la kupitia penati ya dakika za majeruhi iliyofungwa na Samaras tena.
Colombia ilikamilisha mechi za makundi kwa kuiadhibu Japan 4-1 na kuweka rekodi ya kushinda mechi zote katika makundi.


Comments