Timu ya Kagondo FC imejipatia Alama tatu                muhimu kwenye Mtanange wao dhidi ya timu ya Buhembe FC leo                kwenye Uwanja wa Kaitaba Bukoba Mjini kwenye Michuano ya                Kombe la Kagasheki. Bao hilo la pekee lilifungwa na                Mchezaji namba tisa Mgongoni Abduratif Khamis katika                kipindi cha kwanza dakika 37. Kipindi cha kwanza                kilimalizika kwa bao hilo 1-0 na kipindi cha pili timu                zote mbili hakuna iliyoziona nyavu za mwezake timu licha                ya kushambuliana mara kwa mara. Mwamuzi alipuliza kipenga                dakika 90 kumaliza mtanange huo na Timu ya Kagondo FC                wakiibuka na ushindi huo wa bao 1-0. Mapema leo Mchana                Timu ya Nshambya na Kibeta ziliumana na timu zote mbili                zilimaliza mtanange kwa sare ya bila kufungana kwa kutoka                0-0. Kesho Ligi hii inaendelea tena kwa siku ya nne na                kutakuwepo na michezo miwili, Mapema ni Nyanga vs                Kitendaguro na Jioni saa 10:00 ni Wagonga Nyundo                "Ijuganyondo Vs Kahororo".
                Kikosi cha Timu ya Kagondo Fc
                                Kipute kilianza kwa Timu ya Buhembe kwa                kasi sana
        Kipa wa Kagodo chupuchupu afungwe bao hapa                katika kipindi cha pili. Kipindi cha pili hakuna                aliyeziona nyavu za mwenzake bao hilo lilidumu mpaka                dakika za mwisho
                Hatari: Kipa wa Kagondo Fc akidaka mpira wa                Kona
                Kipindi cha Pili dakika za mwishoni Timu ya                Buhembe FC ilipata kona mbili lakini haikuweza kusawazisha                bao, licha ya kuliandama lango la wenzao Kagondo Fc.
                
Comments
Post a Comment