KAGASHEKI CUP 2014 MJINI BUKOBA LEO - KASHAI 3 vs BAKOBA 0,




KAGASHEKI CUP 2014 MJINI BUKOBA LEO - KASHAI 3 vs BAKOBA 0,
Na Faustine Ruta, Bukoba
Michuano ya Kagasheki Cup 2014 imeendelea tena leo kwenye Uwanja wa Kaitaba Bukoba Mjini kwa siku ya pili na kushuhudia mahasimu wawili Mmoja akimliza mwenzake bao 3-0.
Mtanange wa leo hii Jumapili ulizikutanisha timu mbili matata kwenye hii ligi za Kashai na Bakoba FC na kushuhudia Timu ya Bakoba ikifungwa bao 3-0 bao zilizofungwa kipindi cha kwanza mbili na kipindi cha pili moja.
Timu ya Kashai FC walianza kuifunga timu ya Bakoba bao la kwanza katika dakika ya 8 bao likifungwa na Joha Johansen. 
Bao la pili lilifungwa na Msengi Gerard katika dakika ya 38 kipindi cha kwanza na kufanya bao kuwa 2-0 dhidi ya mahasimu wao Bakoba ambao mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika walikuwa hawajapata kitu.
Kipindi cha pili licha ya timu zote mbili kukamiana kwa sana timu ya Bakoba ilipata nafasi kama tatu lakini haikuweza kuifunga timu ya Kashai na hatimaye Kashai kupata bao lao la tatu katika dakika ya 60 kipindi cha pili bao lililotiwa nyavuni na Mchezaji wa Kashai FC Shamte Odilo na Kipute kumalizika kwa dakika 90 Kashai ikiibuka kwa bao 3-0. 
Michuano hii itaendelea tena kesho Jumatatu na kutakuwa na Mitanange miwili wakwanza utachezwa saa nane kati ya Nshambya FC ikiumana na timu ya Kibeta Fc saa 8:00 mchana na mtanange wa saa 10:00 ni baina ya Kagondo Fc na Buhembe Fc.

Dakika 90 zimemalizika waamuzi wanatoka uwanjani ...
Kashai 3 vs Bakoba 0.




Comments