JULIO APITISHWA KUGOMBWA UMAKAMU WA URAIS WA SIMBA SC



JULIO APITISHWA KUGOMBWA UMAKAMU WA URAIS WA SIMBA SC
MWENYEKITI wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC, Dk Damas Daniel Ndumbaro amewapitisha Andrew Peter Tupa na Evans Elieza Aveva kugombea Urais wa klabu hiyo katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Juni 29, mwaka huu, Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mtaa wa Ohio, Dar es Salaam Ndumbaro amesema wagombea hao na wengine wote waliopitishwa sasa wanaruhusiwa kufanya kampeni hadi siku ya uchaguzi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC, Dk Damas Ndumbaro kushoto akitaja wagombea waliopitishwa mchana wa leo. Kulia ni Mjumbe wa Kamati hiyo, Amin Bakhresa.


Ndumbaro amesema katika nafasi ya Makamu wa Rais wamepitishwa watu wanne ambao ni Bundala Kabulwa, Geoffrey Nyange 'Kaburu', Jamhuri Kihwelo 'Julio' na Swedi Mkwabi.
Kkatika nafasi za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji upande wa wanaume wamepitishwa watu 18, ambao ni Said Tulliy, Yasini Mwete, Ally Suru, Rodney Chiduo, Said Pamba, Ally Chaurembo, Abdulhamid Mshangama, Chano Almasi, Damian Manembe, Ibrahim Masoud, Kajuna Noor, Hamisi Mkoma, Alfred Elia, Saidi Kubenea, Idd Mkamballah, Juma Mussa, Maulid Abdallah na Collin Frisch upande wa wanawake wamepitishwa Amina Poyo, Asha Muhaji

na Jasmine Badour
chanzo bin zubeiry





Comments