HII NDIYO MANCHESTER UNITED ANAYOITAKA VAN GAAL … Luke Shaw, Ander Herrera, Arturo Vidal, Alexis Sanchez NDANI …Carrick, Fellaini, Rafael, Phil Jones OUT
MANCHESTER United haitaki kabisa kupoteza muda katika kujenga upya timu yake chini ya kocha Louis van Gaal. Inataka kufanya usajili wenye tija mapema iwezekanavyo badala ya kusubiri ukingoni mwa dirisha la usaji na kupelekea manunuzi ya kukurupuka.
Ikiwa tayari imeshawanasa machipukizi wenye uwezo wa hali ya juu Luke Shaw na Ander Herrera, Van Gaal bado amedhamiria kuongeza nyota wengine ndani ya United ambao watabadilisha kabisa sura ya timu.
Tayari Van Gaal amewaweka Arturo Vidal wa Juventus na Alexis Sanchez wa Barcelona kwenye orodha ya wachezaji anaotaka kuhakikisha wanatua Old Trafford dirisha hili la usajili.
Arturo Vidal (kulia)
Lakini pia Van Gaal yupo pia kwenye mipango ya kuhakikisha anatumia wachezaji wake wa Holland kuimarisha safu ya ulinzi ya United.
Nyota kutoka kikosi cha timu ya Taifa ya Holland anaowataka ni pamoja na beki wa kulia Daryl Janmaat na beki wa kati Bruno Martins. Lakini pia Van Gaal ameonyesha ni ya kuwarudisha Ligi Kuu ya England mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Dirk Kuyt na kiungo wa zamani wa Manchester City Nigel de Jong.
Daryl Janmaat
Hiyo itakuwa inamaanisha kuwa wachezaji Rafael, Phil Jones, Michael Carrick na Marouane Fellaini hawatakuwepo kwenye mipango ya kikosi cha kwanza cha Van Gaal.
Michael Carrick
Comments
Post a Comment