COSTA RICA imetoka sare ya 0-0 na England na kufanikiwa kujikusanyia pointi 7 zinazoifanya iwe kijogoo wa kundi D na kutinga moja kwa moja hatua ya 16 bora.
Kwa matokeo hayo, England imemaliza michezo yake yote mitatu bila kushinda hata mechi moja hii ikiwa ni baada ya kufungwa mechi zake mbili zilizopita.
Uruguay nayo imefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora baada ya kuichapa Italia bao 1-0 katika mchezo mwingine wa kundi B.
Bao la Uruguay ambayo sasa inafikisha pointi tano, lilifungwa na Diego Godin dakika ya 81. Italia sasa inaungana na England kufungasha virago na kurejea nyumbani.
Comments
Post a Comment