BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' AWASHUKURU VIONGOZI WA NGUMI NCHINI

 
BONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' amewashukuru viongozi wa ngumi nchini kwa sapoti yao wanayo mpa tangu ahanze ngumi mpaka sasa kwani yeye malengo yake ni kufika mbali zaidi baada ya kunyakuwa mkanda wa ubingwa unaotambuliwa na WPBF Africa Welterweight Title

Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa DDC Keko kulipokuwa na mkutano mkuu wa chama cha ngumi za kulipwa nchini cha TPBC, ambapo alikutana na viongozi mbalimbali na kupongezwa kwa kunyakuwa mkanda huo wa ubingwa alioupata Zambia kwa kumpiga bondia Mwansa Kabinga kwa TKO ya raundi ya tisa katika uwanja wa Arthur Davies Stadium, Kitwe, Zambia

bondia huyo mwenye ndoto za kuwa mmoja wa mabondia watakotamba duniani ambapo mwanzoni mwa mwaka huu aliteuliwa kuwa bondia bora wa mwaka 2013 katika uzito wake tuzo zilizoanza kufanyika mwaka huu

fikra zake kwa sasa ni kuwa bingwa wa mikanda mbalimbali inayotambulika Duniani katika uzito wake fikra zake siku moja ni kupambana katika mapambano makubwa zaidi hususani katika ukumbi wa MGM Gland nchini Marekani.

Bondia huyo mwenye rekodi ya kushinda mapambano 11 na kupoteza mpambano mmoja wakati ananza mchezo huo.bondia huyo anawashukurujopo la makocha wake wa kambi ya ilala linalo ongozwa na kocha mkongwe wa mchezo huo Habibi Kinyogoli 'Masta',kondo Nassoro,Sakwe Mtulya na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kwa kumsimamia na kumpa ushari anapokuwa ulingoni akipambana

bila kuwasahau mashabiki wake waliojaa kila kona ya jiji la Dar es salaam na Tanzania nzima kwa ujumla

Comments