LICHA ya kukabiliwa na adhabu ya kufungiwa na FIFA kwa miezi minne kwa kumng'ata mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini, Barcelona ya Uhispania haijakata tamaa ya kumsajili mshambuliaji machachari wa Uruguay Luis Suarez.
Mshambuliaji huyo wa kutegemewa wa klabu ya Liverpool ya Uingereza amepigwa marufuku ya miezi minne kumaanisha kuwa hatoshiriki mechi yeyote hadi mwezi mwishoni mwa mwezi Oktoba.
Inadaiwa Liverpool ipo tayari kuumuza mchezaji huyo kama Barcelona watafika bei ya pauni milioni 80.
Katika kujindaa kwa pengo la mchezaji huyo, Liverpool inakamilisha usajili wa kiungo Adam Lallana kutoka Southampton huku pia ikiandaa mipango ya kumnasa winga wa Benfica Lazar Markovic.
Lazar Markovic (kulia) jeshi lipya linalosakwa na Liverpool
Adam Lallana (kulia) yuko njiani kutua Liverpool
Haijulikani kwanini mabingwa hao wa zamani wa kombe la mabingwa barani uropa ambao wanajivunia huduma za Lionel Messi wa Argentina na Neymar wa Brazil bado wanamtaka Suarez.
Liverpool ilimnunua Suarez kwa pauni milioni £25m mwezi Januari 2011 kutoka klabu ya Ajax.
Hii si mara ya kwanza wala hata ya pili kwa Suarez kukabiliwa na kashfa kama hii ya kuwauma wapinzani wake , msimu uliopita alilazimika kukaa nje kwa mechi kumi baada ya kupatikana na hatia ya kumuuma mlinzi wa Chelsea Branislav Ivanovic Aprili 2013.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alirejea kwa kishindo na akaifungia Liverpool mabao 31 na kuisaidia kumaliza katika nafasi ya pili.
Suarez pia aliteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa 2013-2014 .
Nyota huyo wa Uruguay alipokelewa kwa shangwe, vifijo na nderemo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Carrasco huko Montevideo aliporejea nyumbani kutoka Brazil.
Comments
Post a Comment