BAADA ya kuwasajili Ander Herrera na Luke Shaw wiki hii, Manchester United sasa inaelekeza nguvu zake kumnasa kiungo wa Juventus midfielder Arturo Vidal.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile mwenye kudhibiti vema dimba la kati, ameitoa udenda Manchester United ambao tayari wamebisha hodi kujua kama kuna uwezekano wa kumnasa kiangazi hiki.
Msimu uliopita, United chini ya David Moyes ilijaribu kumsajili Vidal lakini ofa yao ikapigwa chini na Juventus.
Kocha mpya wa Manchester United, Louis van Gaal anakusudia kuongeza idadi ya viungo wafumania nyavu kwenye kikosi chake.
Vidal aliifungia Juventus mabao 18 msimu uliopita huku pia akiwa amefunga mara 13 katika kampeni za kuelekea kombe la dunia.
United inaamini dau la pauni milioni 30 linaweza kuwashawishi Juventus kufanya biashara.
Comments
Post a Comment