Algeria                    imefuzu kwa mkondo wa pili wa kombe la dunia
              Algeria                imefuzu kwa raundi ya pili ya kombe la dunia kwa mara ya                kwanza katika historia.
          The Desert Foxes                walitoka nyuma bao moja kwa nunge dhidi ya Urusi katika                kipindi cha kwanza na kusawazisha na hivyo kufuzu kama                mshindi wa pili katika kundi H nyuma ya UbeljijiHii                ndiyo mara yao ya kwanza kupita mkondo wa kwanza.
          Algeria itaingia katika                kumbukumbu za historia ya Soka Afrika kuwa mwakilishi wa 6                kuwahi kufuzu kwa raundi hiyo ya 16 bora nyuma ya Cameroon                Ghana Nigeria Morocco na Senegal .
          Algeria imefuzu kwa                    mkondo wa pili wa kombe la dunia
                Algeria ilikuwa                imefungwa mapema katika kipindi cha kwanza kupitia kwa                mkwaju wake Aleksandr Kokorin aliyepata pasi murua kutoka                kwa Dmitri Kombarov.
          Hata hivyo vijana wa                kocha Fabio Capello walianza kulinda ngome yao mapema bila                ya tahadhari kuwa baop lolote la Algeria ingewarejesha                nyumbani.
          Mashambulizi ya Algeria                yalizaa matunda kunako dakika ya 60 Islam Slimani                alipoisawazishia Algeria kutokana na mkwaju wa freekick                uliopigwa na Yacine Brahimi.
          Wadau watachunguza tukio                ambalo shabiki mmoja anadaiwa kumulika kifaa cha Laser                usoni mwa kipa wa Urusi Igor Akinfeev kabla ya bao hilo la                kusawazisha.
          Algeria imefuzu kwa                    mkondo wa pili wa kombe la dunia
                Kocha Capello                amelalamikia hatua ya refarii kupuuza tukio hilo akisema                kuwa huenda marefarii wananjama ya kuihujumu timu ya                Urusi.
          Urusi ilifanya                mashambulizi kwenye lango la Algeria la Algeria lakini                wapi safu ya ulinzi ilikaa ngangari na kuhimili                mashambulizi hadi kipenga cha mwisho na hivyo kuipa                Algeria alama moja muhimu iliyoiwezesha kuweka historia ya                kufuzu kwa raundi ya pili ya kombe la dunia.
          Algeria sasa imeratibiwa                kukwaruzana na Ujerumani katika mechi ya 16 bora siku ya                jumatatu.Chanzo BBC Swahili
        
Comments
Post a Comment