ALGERIA YAFUATA NYAYO ZA NIGERIA 16 BORA … tatu za Afrika zaaga, mbili zavuka



ALGERIA YAFUATA NYAYO ZA NIGERIA 16 BORA … tatu za Afrika zaaga, mbili zavuka

Up for it: Algeria's Islam Slimani rises above                  Russia's goalkeeper Igor Akinfeev to score

ALGERIA imetinga 16 bora ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza kwenye historia yao ya soka baada kutoka sare ya 1-1 na Urusi.

Bao la kichwa la Slimani ambalo lilikuwa la kusawazisha, likatosha kuwapatia wawakilishi hao wa Afrika pointi moja waliyokuwa wanahitaji ili kuvuka.

Urusi inayofundishwa na Fabio Capello, kocha anayelipwa zaidi kuliko makocha wote wa Kombe la Dunia, imeaga michuano baada ya kuambulia nafasi ya tatu.

Vijana wa Capello ambao ili kusonga mbele walikuwa wanahitaji ushindi, walipata bao la kuongoza dakika ya sita kupitia kwa Aleksandr Kokorin kabla ya Slimani kusawazisha dakika ya 60.

Ubelgiji ndio vinara wa kundi H kwa kujikusanyia pointi 9 baada ya kuinyuka Korea Kusini 1-0. Algeria ina pointi 4, Urusi pointi 2 na Korea Kusini pointi 1.

Mapema kabla ya michezo hiyo ya kundi H, Ghana iliaga michuano kwa kufungwa 2-1 na Ureno.

Timu mbili za Afrika (Nigeria na Algeria) zimevuka na tatu (Ivory Coast, Cameroon na Ghana) zimeaga michuano.



Comments