YAYA Toure ameongeza mafuta kwenye moto aliouwasha juu ya uwezekano wa kutimka Manchester City kiangazi hiki baada ya kuweka wazi kuwa itakuwa heshima kubwa kwake kuichezea Paris Saint-Germain.
Kiungo huyo amekuwa kwenye wakati mgumu baada ya wakala wake kuzungumzia namna mmiliki wa klabu alivyomkosea heshima katika birthday ya mchezaji wake kutimiza miaka 31 ya kuzaliwa wiki mbili zilizopita.
Alipoulizwa juu ya uwezekano wa kujiunga na mabingwa wa Ufaransa, Toure alikuwa mbali na utata kwenye majibu yake.
"Wakati ninapofikiria kuhusu muundo wa PSG, ni vipi hutavutiwa na klabu kama hiyo? Toure alisema katika maongezi yake na France Football.
"PSG imejitokeza kuwa timu yenye nguvu barani Ulaya. Itakuwa ni heshima siku moja mimi kuwa sehemu ya klabu hiyo ...kama ikibidi"
Comments
Post a Comment