Wakazi wawili wa Dar es Salaam wamejishindia tiketi za kwenda nchini Brazil kuona moja ya mechi za kombe la Dunia kupitia promosheni ya Kwea Pipa na televisheni ya Taifa ya TBC kwa kushirikiana na kampuni ya Push Mobile Media Limited.
Washindi hao ni Donald Milinde Shija (34) mkazi wa Mabibo jijini ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya Davis and Shirtliff na mshindi mwingine ni Shaban Athumani Saidi (22) mkazi wa Banana-Kitunda ambaye ni fundi pampu.
Kaimu Mkurugenzi wa TBC, Suzan Mungy alisema kuwa washindi hao wamepata baada ya kutuma neno 'Kombe' kwenda namba 15522 na kushinda nafasi ya kuona mechi kali kati ya wenyeji Brazil na Cameroon June 23.
Alisema kuwa jumla ya watanzania watano watapata nafasi ya kuona mechi hiyo na kwa sasa bado watanzania watatu kupata tiketi hizo za kwenda kuwaona wachezaji nyota wa Cameroon kama Benoit Assou-Ekotto, Alex Song na Samuel Eto'o na yule wa Brazil kama vile Neymar da Silva Santos JĂșnior, Thiago Silva, Dan Alves na wengine wengi.
Meneja kampeni wa promosheni hiyo ya Semu Bandora kutoka kampuni ya Push Mobile Media Limited alisema kuwa droo nyingine ya promosheni hiyo itafanyika wiki ijayo na mbali ya tiketi, kuna zawadi mbali mbali ambazo zitatolewa kwa washindi.
"Kuna zawadi za ving'amuzi zaidi ya 250, televisheni za flat screen sita na fedha taslimu, tunawaomba watu washiriki zaidi ili katika promosheni hii na kushinda moja ya zawadi pamoja na ile kubwa ya tiketi," alisema Bandora.
Comments
Post a Comment