WANACHAMA SIMBA SC OGOPENI `SIASA NYEPESI` MITHIRI YA UKOMA WAKATI HUU WA UCHAGUZI, KUMBUKENI HAYA….



WANACHAMA SIMBA SC OGOPENI `SIASA NYEPESI` MITHIRI YA UKOMA WAKATI HUU WA UCHAGUZI, KUMBUKENI HAYA….
Wanachama-SimbaNa Baraka Mpenja wa fullshangweDar es salaam
WANACHAMA wa Simba sc kuna mambo mengi yanayoendelea kuelekea uchaguzi mkuu wa klabu yenu utakaofanyika juni 29 mwaka huu, hasa baada ya mgombea mmoja wa Urais, Michael Richard Wambura kuenguliwa kutokana na sababu tofauti.
Kuenguliwa kwa Wambura na kamati ya uchaguzi wa Simba chini ya mwenyekiti wake, mwanasheria na wakala wa wawachezaji wa FIFA, Dkt. Damas Ndumbaro kunaonekana kuvuta hisia za wadau wengi wa soka na wanachama wa Simba wenye mapenzi makubwa kwa mgombea huyu.
Ni dhahiri wapo wanachama wengi wenye mapenzi makubwa kwa Wambura na piga ua galagaza wao wanajua kiongozi anayeifaa Simba kwa sasa ni huyo.
Lakini kumbuka pia kuwa wagombea wengine, Evans Aveva na Andrew Tupa. Wote hawa wanaungwa na watu wengi nyuma yao. Lakini yawezekana sababu zikatofautiana.
Aveva ana wapenzi wengi wanaohitaji kumuona katika kiti cha Urais wa Simba kuanzia juni 29 mwaka huu. Ni dhahiri kuwa Aveva ni moja ya wagombea wenye nguvu kwenye uchaguzi huu.
Ushahidi wa mamia ya mashabiki waliomsindikiza kuchukua fomu na kurudisha fomu unatosha kuamini kuwa Aveva anaungwa mkono na wanachama wengi, ingawa bado si rahisi kujiridhisha kuwa wote wale ni wanachama halali wa Simba.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com


Comments