Kamati ya Uchaguzi chini ya mwanasheria, Damas Ndumbaro iliwaweka kitimoto wagombea wote waliowekewa mapingamizi huku pingamizi la Kaburu likionekana kuwa ngoma nzito zaidi kwa mgombea huyo.
Kaburu aliwekewa pingamizi na mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, Ather Mwambeta (kadi namba 01005), ambaye alidai Kaburu akiwa Makamu Mwenyekiti alikiuka katiba ya Simba ibara ya 33 (5) na 28 (1b) kwa kushindwa kuwasilisha ripoti ya mapato na matumizi ya fedha katika mkutano mkuu wa 2010 hadi 2013 alipojiuzulu.
Kwa upande wa Wambura, ameongoza kuwa na mapingamizi mengi zaidi (matano) aliyowekewa na wanachama Swalehe Madjapa, Daniel Kamna, Said Rubeya 'Seydou', Ustadh Masoud na Chacha.
Akizungumza na gazeti hili jana, Wambura alisema: "Nimesikiliza mapingamizi yangu, hoja zote zilizotolewa na walioniwekea pingamizi ni zile zile za miaka yote, hakuna mpya, wote wamekuja na hoja moja ya kwenda mahakamani na mimi nimezijibu kwa hoja."
Comments
Post a Comment