WAKALI WAO YA THABIT ABDUL KUZINDULIWA RASMI LEO …Khadija Kopa, Jokha, Baikoko, Misambano, Msagasumu kusindikiza

HATIMAYE kundi jipya la taarab, Wakali Wao Modern Taradance chini ya Thabit Abdul, linazinduliwa rasmi leo katika ukumbi wa Travertine.

Lakini Wakali Wao hawaendi watupu Travertine, bali wanaandamana na albam yao ya kwanza "Kalieni Viti Siyo Umbeya" ambayo nayo pia itazinduliwa rasmi leo.

Uzinduzi huu ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa, utasindikizwa na wasanii nyota Khadija Kopa, Jokha Kassim, Abdul Misambano na Msagasumu.

Kama vile hiyo haitoshi, wale wakali wa nyonga, Baikoko Original chini ya Super Maya, nao pia watasindikiza uzinduzi wa Wakali Wao.

Je Thabit ataingia vipi ukumbini? Ni suala la kusubiri.

Comments