Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa(kushoto)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusiana na uzinduzi wa huduma ya"Global Sport"kwa wa wapenzi wa michezo nchini kuweza kupata habari mbalimbali bure kwa siku(15)za mwanzo kupitia simu zao za mkononi mahali popote na muda wowote ili kujiunga mteja anatakiawa kuandika neno SPORT au SPORTS kwenda namba 15778,katikati ni kocha msaidizi wa simba Seleman Matola na Afisa huduma za ziada wa kampuni hiyo Mathew Kampambe.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika uzinduzi wa huduma ya"Global Sport"iliyozinduliwa na Mtandao wa Vodacom unaoongoza Tanzania kwa wa wapenzi wa michezo kuweza kupata habari mbalimbali bure kwa siku(15)za mwanzo kupitia simu zao za mkononi mahali popote na muda wowote ili kujiunga mteja anatakiawa kuandika neno SPORT au SPORTS kwenda namba 15778.
Huku zikiwa zimesalia siku chache kuanza kwa kombe la Dunia Nchini Brazil, wapenzi wa michezo nchini sasa wamerahisishiwa kupata habari mbalimbali kupitia simu zao za mkononi mahali popote na muda wowote kufuatia kuzinduliwa kwa huduma mpya ya Global Sport .
Akizungumzia juu ya huduma hiyo Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Kelvin Twissa amebainisha kuwa watanzania wengi wanapenda michezo lakini kutokana na miundombinu hafifu ya upashanaji wa habari mambo mengi huwa yanawapita.
"Global Sport ni huduma nyingine mpya kabisa kutoka Vodacom ambayo itamwezesha mteja kupata taarifa juu ya mchezo wa za soka kutoka ligi mbali mbali duniani ikiwemo VPL na hususani michuano ya kombe la dunia ikiwa imebakiza siku chache kabla ya kuanza kutimua vumbi nchini Brazil. Mbali na soka pia kutakuwa na habari za uhakika na kuaminika za michezo kama vile mpira wa kikapu, kriketi na mingineyo mengi itakuwa ikipatikana ndani ya huduma hii." Alisema Twissa.
Alisema kuwa "Ni ukweli usiopingika kwamba kila mmoja wetu anakuwa na aina ya mchezo anaoupenda na kuufuatilia kwa karibu sana. Vodacom kwa kuligundua hilo, tumeamua kuwawezesha wapenda michezo wote nchini kupata habari zinazojiri katika michezo wanayoipenda. Tunalifanikisha hili kwa lengo la kuweza kuwarahisishia wateja wetu na wapenzi wa michezo kwa ujumla hapa nchini." Aidha Twissa amefafanua kuwa ili mteja aweze kujipatia huduma hiyo itambidi ajiunge kwa kuandika neno SPORT au SPORTS kwenda namba 15778 ambapo kwa siku 15 za mwanzo huduma hii itakuwa ni bure kabisa. Pia kama mteja atataka kujitoa itamlazimu atume ujumbe wenye neno STOP kwenda namba hizohizo alizojiunga nazo yaani 15778.
"Siku zote Vodacom huwa tunakuwa wabunifu kugundua ni nini wateja wetu wanakihiaji na hatuko tayari kuona wakipata wakati mgumu wakati uwezo na teknolojia tunazo kukidhi haja zao. Kuzinduliwa kwa Global Sport sasa kutamuwezesha mtu hata aliyeko huko Sumbawanga kupata nini kunachojiri katika ulimwengu wa soka nchini ili mradi ni mteja wa Vodacom na siyo kusubiria mpaka gazeti lisafirishwe kutoka Dar es Salaam ambalo linaweza kuchukua mpaka siku tatu kumfikia." Alimalizia Twissa.
Nae kwa upande wake kocha Masaidizi wa Simba Sports Club, Selemani Matola alihitimisha kwa kusema "huduma hii imekuja wakati muafaka cha msimu wa kombe la dunia ambapo watanzania wanahaja kubwa yakujua habari mbali mbali kuhusu kombe hilo. Hivyo nawashauri watumie huduma iyo ipasavyo ili kuweza kwenda na wakati na kujua kinachoendelea katika ulimwengu wa soka".
Comments
Post a Comment