ULE UHONDO WA MASHUJAA BAND NI LEO USIKU …Kalunde Band kusindikiza, kilaji na vitafunwa mpaka baaasi!
HATIMAYE lile onyesho la kihistoria kutoka kwa bendi bora ya muziki wa dansi kwa mwaka wa pili mfululizo, Mashujaa Band, limewadia na mambo yote ni leo Ijumaa usiku ndani ya ukumbi wa Letasi Lounge (zamani Busness Park) Victoria jijini Dar es Salaam.
Onyesho hilo litasindikizwa na Kalunde Band chini ya Captain Deo Mwanambilimbi.
Kama ilivyoelezwa hapo awali Moja ya lengo kuu la onyesho hilo, ni kupongezana kwa wote waliochangia mafanikio ya Mashujaa Band kuanzia ilipotoka hadi sasa, hii ikiwa ni pamoja na tuzo tatu za Kili Music Awards ilizonyakua mwaka huu.
Meneja Masoko wa Mashujaa Band, Max Luhanga aliiambia Saluti5 kuwa onyesho hilo litakutanisha watu wa vyombo vya habari, mashabiki wa Mashujaa na wapenzi wa muziki wa dansi kwa ujumla wake ambapo watakunywa pamoja, kutafuna nyama choma pamoja huku wakiburudika na muziki kutoka kwa Kalunde Bana na Mashujaa Band.
Comments
Post a Comment