Tanzia:Bongo Movie yapata pingo jingine; Recho afariki...!




Tanzia:Bongo Movie yapata pingo jingine; Recho afariki...!

RECHO AFARIKI: Msanii Rachel Haule 'Recho' afariki asubuhi hii Muhimbili Hosp, Dar baada kujifungua kwa upasuaji. Mtoto alifariki jana, Bongo Movie yathibitisha

Recho alikwenda Muhimbili jana kujifungua ambapo mara baada ya kujifungua mtoto alifariki na yeye hali yake kuwa mbaya, ilibidi ahamishiwe ICU ambako hali ilizidi kuwa mbaya na baadae kufariki dunia.

Kifo cha Recho kimekuja ndani ya wiki moja baada ya kufariki kwa msanii mwingine wa Bongo Movi Adam Kuambiana Jumamosi iliyopita, kifo hiki kimeleta mstuko mkubwa kwenye tasnia ya ya filamu za kibongo. Habari na picha zaidi zitawajia baadae.

Comments