SUAREZ AWAPIGA `CHANGA LA MACHO` REAL MADRID, BARCELONA, ASEMA YEYE `GADO KWA GADO` NA LIVERPOOL YAKE
Imechapishwa Mei 27, 2014, saa 9:34 asubuhi
LUIS Suarez amemwambia mchezaji mwenzake wa Liverpool kuwa ana mpango wa kubakia klabuni hapo msimu ujao ili kuisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi kuu soka nchini England.
Jana jumatatu, Liverpool walisema kuwa kocha mkuu Brendan Rodgers amesaini mkataba mpya utakaomuweka Anfield mpaka mwaka 2018 na atapata nguvu zaidi kwa uwepo wa Suarez.
Ripoti zinasema Real Madrid wameweka dau la paundi milioni 100 kwa ajili ya kuinasa saini ya Suarez ambaye alisaini mkataba mrefu na Liverpool mwezi desemba mwaka jana na aliahidi kukaa muda mrefu klabuni hapo.
Lakini vyanzo vya habari Bernabeu vinaeleza kuwa hakutakuwa na haja ya kumsajili Suarez kama Karim Benzema atakubali kusaini mkataba mpya.
Mfaransa huyo ambaye yuko kwenye rada za Arsenal anahitaji kuongezewa dau na Real Madrid, lakini klabu hiyo inaamini watafikia makubaliano na nyota huyo mwenye miaka 26 kabla ya kombe la dunia.
Comments
Post a Comment