SANTIAGO BERNABEU YAZIZIMA, REAL MADRID WAANGUSHA BONGE LA PARTY …mashabiki 80,000 wajazana uwanjani
REAL MADRID iliwaalika mashabiki wake katika uwanja wa Santiago Bernabeu Jumapili usiku ili kusherehekea ushindi wa kihistoria wa ubingwa wa Ligi wa Mabingwa ikiwa ni mara yao ya kumi.
Zaidi ya mashabiki 80,000 wakajazana kwenye uwanja huo masaa 24 baada ya vijana wa Carlo Ancelotti kutawazwa kuwa mabingwa wapya.
Real Madrid waliwazima watani wao mji mmoja, Atletico Madrid katika muda wa ziada kwenye fainali iliyofanyika Stadium of Light huko Lisbon Ureno ambapo matokeo yalikuwa ni 4-1.
Atletico waliongoza hadi dakika ya mwisho ya mchezo kabla Real Madrid hawajazawazisha na kulazimika kuongezwa dakika 30 za nyongeza zilizoshuhudia karamu ya magoli.
Comments
Post a Comment