QPR SASA YAJIANDAA KUWASAJILI FRANK LAMPARD NA RIO FERDINAND



QPR SASA YAJIANDAA KUWASAJILI FRANK LAMPARD NA RIO FERDINAND

FBL-EUR-C1-MAN UTD-OLYMPIAKOS

QPR inataka kuongeza uzoefu kwenye kikosi chake baada ya kurejea Ligi Kuu ya England ambapo sasa wanakusudia kuwasajili wakongwe Frank Lampard na Rio Ferdinand.

Kocha wa timu hiyo Harry Redknapp ameripotiwa kuwa anahitaji sura mpya sita – lakini uzoefu ndio kipaumbele chake na hiyo ndio sababu ya kuwataka Lampard na Rio waliotemwa na timu zao za Chelsea na Manchester United.

FBL-WC-2014-ENG-TRAINING

Redknapp aliwahi kufanya kazi na wachezaji hao enzi zake za ukocha wa West Ham. Wote wawili wana umri wa miaka 35.

Lampard anatarajiwa kupewa mkataba wa mwaka mmoja lakini pia kukiwa na uwezekano wa kuongezewa miezi 12 zaidi, wakati Rio atapewa mkataba wa kuitumikia QPR hadi mwezi Januari na baada ya hapo atakuwa huru kwenda kujiunga na ligi ya Marekani MLS kama atapenda.



Comments