NEW YORK YAPATA KIPIGO CHA MBWA MWIZI, YAPACHIKWA 5-0 NA DMV, PBZ WADHAMINI MECHI HIYO



NEW YORK YAPATA KIPIGO CHA MBWA MWIZI, YAPACHIKWA 5-0 NA DMV, PBZ WADHAMINI MECHI HIYO
Timu ya New York
Timu ya DMV
 Mwakilishi wa mgeni rasmi Afisa Suleiman Saleh akisalimiana na refa Mohammed.

Timua New York siku ya Jumamosi ilizima fegi mbele ya timu ya DMV kwenye mtanange uliokuwa ukisubiliwa kwa hamu na mashabiki wa DMV wakiongozwa na wachezaji wa timu zote mbili kwa kutambiana kwenye mitandao ya kijamii kabla ya mtanange huo kuhitimishwa hapo jana siku ya Jumamosi May 24, 2014 katika uwanja wa Walker Mills Park uliopo Capitol Heights.

Mbali na mechi hiyo kuwa nzuri na ya kuvutia iliingia dosali pale ilipochelewa kuaanza baada ya muhudumu wa uwanja kuchelewa kufungua geti la kuingilia uwanjani kwa madai ya kutokuwa na taarifa zozote za kukodishiwa uwanja kwa siku hiyo ya Jumamosi na kupelekea mgeni rasmi Mhe. Liberata Mulamula, Balozi wa Tanzania nchini Marekani kuondoka kuelekea kwenye majukumu mengine ambayo siku hiyo ya Jumamosi pia alikua ni mgeni rasmi kwenye mkutano wa dini uliokuwa inafanyikia Hampton Inn, College Park na Balozi Liberata Mulamula kumkabidhi majukumu ya ugeni rasmi kwa Afisa Ubalozi Suleiman Saleh.

Mechi hii ambayo ilikuwa imepaniwa na wachezaji wa timu zote mbili ilianza taratibu kwa timu ya New York kuanza kutandaza soka ya kitabuni kwa pasi fupi fupi na za fisigino na kujaribu kulitia msukosuko goli la DMV mara kwa mara huku wachezaji wakongwe wa DMV waliochanganyika na wachezaji wachache damu changa wakiendelea kusoma mchezo wa wapinzani wao.

Mchezo ulionekana kama ungekua wa nguvu sawa kutokana na timu zote kushindwa kumalizia pasi za kufunga mabao kwa washambuliaji wa timu zote kupiga nje au kumlenga mlinda mlango. Mechi hiyo pia ilionekana kama timu zote zingeenda mapumziko bila kufungana lakini mambo yalibadilika kunako dkk ya 35 mchezaji wa DMV David Nduguru alipopachika bao safi kwa shuti kali ndani ya 18 baada ya kupokea pasi toka kwa mchezaji Vincent Ndusilo naye mfingaji kuuweka mpira kimyani bila ajizi na kufanya timu ya New York kucheza kwa kushambulia kama mbogo aliyejeruhiwa na kujaribu kutafuta bao la kusawazisha bila mafanikio.

Dakika moja kabla ya mapunziko David Ndunguru alipachika bao la pili baada mabeki wa timu ya New York wakidhani ameotea na mpira kumkuta mfungaji akiwa peke yake na kipa na kupiga shuti lingine kali na kumchambua kipa Salimu ambaye alikua akiwapigia makelele wachezaji wake karibu muda waote wa mchezo, Mprira ulienda mapumziko huku timu ya DMV ikiwa mbele kwa bao 2-0 dhidi ya timu ngumu ya New York yenye wachezaji wenye umri mdogo ukilinganisha na DMV. Pia katika kipindi hicho cha kwanza timu ya New ilipata pigo baada ya beki wake wa kutumainiwa NY Ebra kuumia na kutoka inje na baadae kukimbizwa hospitali baada ya kubambikwa na mchezaji wa DMV na kusababisha ugoko wake mguu wa kulia kupata ufa. Kwa sasa NY Ebra anaendelea vizuri .

Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko lakini mabadiliko hayo yalionyesha kuinufaisha timu ya DMV kwani ilipoingia kipindi cha pili ilianza kwa kasi kubwa na kulishambulia goli la New York kama nyuki pengine kuumia kwa beki NY Ebra kuliinufaisha timu ya DMV kwani wachezaji wake mbele walionekana wenye uhai katika kipindi hiki chapili kuliko kile cha kwanza. Mchezaji wa siku nyingi aliyeingia kipindi cha pili Dullah Riyami aliipatia DMV bao la tatu  lililozima nguvu ya timu ya New York bao hili lilipatika katika dkk ya 65 ya mchezo.

Dkk ya 74 ya mchezo ni Dullah tena aliyepigilia msumari mwingine kwnye jeneza la magaoli kwenye tumu hii ya New York ambayo kabla ya mechi kuanza ilionekana kama wao ndio wangeibuka mshindi kwani walikua na historia nzuri baada ya kuwafunga Massachusetts 7-1 kwenye mechi yao ya kwanyza iliyofanyika New York.


Kunako dkk ya 82 mchezaji Dedi Luba alifunga kitabu cha magoli baada ya kupachika bao safi baada ya kupokea pasi safi na yeye kuungangisha crosi hiyo moja kwa moja iliyotoka upande wa kulia ya uwanja. Mpaka dkk 90 kuisha DMV 5- New York 0


Comments