NDOVU SPECIAL MALT YASHINDA TUZO YA UBORA WA KIMATAIFA 2014 KATIKA TUZO ZA MONDE SELECTION




NDOVU SPECIAL MALT YASHINDA TUZO YA UBORA WA KIMATAIFA 2014 KATIKA TUZO ZA MONDE SELECTION
Meneja wa Biaya Ndovu Special Malt, Pamela Kikuli (kushoto) akizungumza na waandishi w ahabari (hawapopichani)kuhusu tuzo iliyopata hivi karibuni ya ubora wa kimataifa. Kulia ni Meneja masoko wa Kampun iya Bia Tanzania (TBL), Fimbo Butallah.





Meneja masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Fimbo Butallah (kulia). Akizungumza na waandishi wa habari (hawapopichani) kuhusu tuzo iliyopata hivikaribu ni ya ubora wakimataifa.

 Bia ya Ndovu yazidi kupata umaarufu katika ngazi za kimataifa kwani imezawadiwa tuzo la Ubora wa Kimataifa kwa mwaka 2014 ijulikanayo kama 'International High Quality Trophy 2014'.
 



 

 Ndovu itapokea tuzo hiyo katika hafla itakayo fanyika Jumatatu 2 Juni 2014, mjini Bordeaux, Ufaransa.


 

Kwa zaidi ya miaka 3 mfululizao bia ya Ndovu Special Malt imekuwaikishinda tuzo za 'Gold' na 'Grand Gold' iliyopelekea kuzawadiwa kombe la ubora wa Kimataifa 2014.


 



 

Akizungumza na waandishi wa Habari, Meneja wa Bia ya Ndovu Bi. Pamela Kikuli alisema, "Ni heshima kubwa sana kwetu kutambuliwa katika ngazi za kimataifa. Tuzo hii inatupa motisha wa kuzidi kuimarisha ubora wa Ndovu Special Malt, kuongeza ubora ili kuwaburudisha wateja wetu ziadi".


 



 

"Tunafurahi sana kuweza kuiipa bia ya Kitanzania umaarufu duniani kutokana na ubora wake. Tungependa kuishukuru Monde Selection kwa kuaanda shindano hili ambalo linatambua na kuzawadia kilicho bora. Tuzo hii sio tu kwa TBL Ndovu Special Malt, bali ni kwa Tanzania nzima" alisema Bw. Fimbo Butullah, Meneja wa Masoko Bia ya Ndovu.


Comments