Jhikoman akikamua ughaibuni
Jhikoman aliwasili Finland tarehe 24.4.2014 kuanza ziara ya kimuziki katika nchi za Ulaya
Nchini Finland katika amefanya maonyesho sita!
Kubwa ni lile alilolifanya Helsinki African Film Festival 16.5.2014
na pia alifanya onyesho la utangulizi kabla ya mkongwe Peetah Morgan wa Morgan Heritage kupanda
jukwaani 23.5.2014. 10.5.2014 alifanya onyesho kwenye uzinduzi wa Helsinki African Film Festival!
Jhikoman amefanyakazi studio na msanii mashuhuri wa Hip hop nchini Finland Paleface!
Kwa sasa Jhikoman yupo studio akiandaa nyimbo aliyo mshirikisha Peetah Morgan.
Tarehe 4 june 2014 Jhikoman anategemea kutumbuiza Kwenye ukumbi wa Nordic Black Theater mjini Oslo nchini
Norway. Jhikoman pia anatarajia kudhuru miji ya Brussels Ubeligiji, Paris Ufaransa, Tübingen Germany,
Stockholm Sweden na Copenhagen Denmark
Jhikoman akiongoza mashambulizi FinlandJhikoman and Peetah MorganMwanamuziki Nyota wa Jamaika Peetah Morgan alikuwa jukwaani na Jhikoman
Comments
Post a Comment