MHESHIMIWA SUGU KWA HILI UMETELEZA …kutoa pole kwa Kuambiana na Recho huku ukiwasahau Gurumo na Amina Ngaluma ni kioja

MBUNGE wa Mbeya mjini Mheshimiwa Joseph Mbilinyi "Sugu" amedhihirisha namna muziki wa dansi unavyochungulia kaburi.

Akichangia bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Alhamisi asubuhi, Sugu alianza kwa kutoka pole kwa wasanii waliofariki hivi karibuni.

"Napenda kutoa pole kwa wasanii waliofariki: Adam Kuambiana na Recho Haule."

Sugu ambaye ni mwanamuziki nguli wa muziki wa kizazi kipya, hakuweza kumkumbuka gwiji la muziki wa dansi, Muhudin Maalim Gurumo aliyefariki kiasi cha siku 50 zilizopita.

Lakini pia Sugu hakukumbuka kifo cha mwimbaji nyota wa kike wa muziki wa dansi Amina Ngaluma aliyefariki siku chache kabla ya kifo cha Adam Kuambiana.

Hii maana yeke ni moja. Muziki wa dansi na wanamuziki wa dansi hawapo kichwani mwa mheshimiwa Sugu.

Kumekuwa na kilio kikubwa kuwa muziki wa dansi unafukiwa na vyombo vya habari, lakini alichokifanya Mheshimiwa Sugu kinadhihirisha kuwa wapo wengi, tena wenye dhima kubwa wanaouweka muziki huo kapuni.

Angalau Mbunge wa viti maalum kupitia CCM, Esther Bulaya yeye alimkumbuka Mzee Gurumo wakati akichangia bajeti ya wizara hiyo.

Comments