MBWANA SAMATTA HATIHATI KUWAVAA ZIMBABWE JUMAPILI, ANASUMBULIWA NA MAJERUHI YA NYAMA ZA PAJA


10418977_738351759562105_7960579550010362518_nNa Baraka Mpenja, Dar es salaam
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania anayeichezea klabu ya TP Mazembe ya DR Congo, Mbwana Ally Samatta yuko hatihati kuichezea timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars katika mchezo wa marudiano kesho kutwa (jumapili) dhidi ya Zimbabwe, mjini Harare,  kuwania kupangwa hatua ya makundi kusaka tiketi ya kushiriki kombe la mataifa ya Afrika, AFCON mwakani nchini Morocco.

Taarifa za uhakika ni kwamba Samatta alipata majeruhi ya nyama za paja katika mechi ya ligi ya mabingwa barani Afrika mei 25 mwaka huu dhidi ya wapinzani wao AS Vita mjini Lubumbashi, huku akifunga bao pekee katika ushindi wa TP Mazembe wa bao 1-0. Katika mchezo huo, Samatta alitolewa dakika ya 75 kutokana na majeruhi hayo.
Hata hivyo imeelezwa kuwa shirikisho la soka Tanzania, TFF, baada ya kuambiwa na TP Mazembe kuwa Samatta ni majeruhi, wao walilazimisha kumtumia mchezaji huyo.
Ili kusoma mahojiano yote yaliyofanyika baina ya mwandishi na meneja wa Samatta bofyawww.bkmtata.blogspot.com


Comments