Na Baraka Mpenja
TP MAZEMBE wamefanikiwa kushinda mchezo wao wa kwanza wa liigi ya mabingwa barani Afrika hatua ya makundi baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 leo hii dhidi ya wapinzani wao wakubwa, AS Vita.
Mchezo huo uliovuta hisia za mashabiki wengi nchini DR Congo umepigwa mjini Lubumbashi.
Bao pekee la ushindi kwa TP Mazembe limefungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta katika dakika ya 62.
Hata hivyo, Samatta aliyeanza katika mechi leo alitolewa mnamo dakika ya 82 na nafasi yake kuchukuliwa na Jonas Sakuwaha.
Katika mchezo wa leo Thomas Ulimwengu alianzia benchi na kuingia dakika ya 67 kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Rainford Kalaba.
Mabadiliko hayakuweza kuleta mabadiliko makubwa katika ubao wa matangazo.
Comments
Post a Comment