BAADA ya Mauricio Pochettino kutambulishwa rasmi kuwa kocha mpya wa Tottenham siku ya Jumanne, SOUTHAMPTON inahofia kuwa kocha wao huyo waliyekuwa nae msimu ulioisha, atajaribu kuwaghilibu wachezaji wao tegemeo.
Pochettino, 42, raia wa Argentina, amesaini mkataba wa miaka mitano, ukiwa na thamani ya pauni milioni 3.5 kwa msimu. Amerithi nafasi ya Tim Sherwood aliyetimuliwa mapema mwezi huu.
Kocha huyo ambaye anatarajiwa kumfanya mshambuliaji Jay Rodriguez wa Southampton kuwa lengo lake kuu katika usajili, alisema: "Hii ni klabu yenye historia ya kipekee na ni heshima kwangu kupata nafasi ya kuwa kocha mkuu hapa. Kuna vipaji vya hali ya juu na ninajiapanga namna kuanza kazi yangu mpya
Comments
Post a Comment