KATIKA mwendelezo mwingine wa burudani, bendi bora ya dansi, Mashujaa Band, Jumatano hii watakuwa na onyesho maalum la Usiku wa Grants.
Onyesho hilo litafanyika Flamingo Night Club Magomeni Mwembechai, jirani na petrol station ya Super Star kuanzia saa 12 jioni hadi usiku mnene.
Meneja Masoko wa Mashujaa Band, Max Luhanga ameiambia Saluti5 kuwa hilo ni onyesho maalum lililodhaminiwa na kinywaji cha Grants.
Max Luhanga anafafanua zaidi: "Ni Sherehe maalum zitakazohudhuriwa na wamiliki wa pombe hiyo ya Grants kutoka Uholanzi.
"Si onyesho la kawaida, ni bonge la party ambapo watu watakata 'kilaji' cha Grants bure, ni kunywa mpaka baaasi.
"Lakini sio kunywa tu bali pia watu watapata burudani kali ya Mashujaa Band ambapo zitaporomoshwa nyimbo kali tupu - mpya na za zamani."
Pichani juu ni mmoja wa marapa hatari wa Mashujaa, Sauti ya Radi
Comments
Post a Comment