MASHUJAA BAND WAJA NA BONGE LA ONYESHO LETASI LOUNGE IJUMAA HII ...ni party ya kupongezana kwa mafanikio ya bendi
BENDI bora ya muziki wa dansi kwa mwaka wa pili mfululizo, Mashujaa Band, Ijumaa hii watakuwa na onyesho la kihistoria katika ukumbi wa Letasi Lounge (zamani Busness Park) Victoria jijini Dar es Salaam.
Moja ya lengo kuu la onyesho hilo, ni kupongezana kwa wote waliochangia mafanikio ya Mashujaa Band kuanzia ilipotoka hadi sasa, hii ikiwa ni pamoja na tuzo tatu za Kili Music Awards ilizonyakua mwaka huu.
Meneja Masoko wa Mashujaa Band, Max Luhanga ameiambia Saluti5 kuwa onyesho hilo litakutanisha watu wa vyombo vya habari, mashabiki wa Mashujaa na wapenzi wa muziki wa dansi kwa ujumla wake ambapo watakunywa pamoja, kutafuna nyama choma pamoja huku wakiburudika na muziki mtamu wa bendi pendwa.
Aidha, Max amesema kuwa baada ya onyesho hilo, Mashujaa Band itakuwa ikiendelea kupatikana Letasi Lounge kila Ijumaa. "Kuanzia Ijumaa hii, Letasi Lounge ndio utakuwa ukumbi wetu wa nyumbani kwa kila Ijumaa," alifafanua.
Comments
Post a Comment