ILIKUWA ni kama onyesho la kuwatoa shaka wale wote wenye mashaka na tuzo zao tatu za Kilimanjaro Tanzania Music Awards. Mashujaa Band wakaangusha show ya kutakata ndani ya Letasi Lounge.
Lilikuwa ni onyesho la kushukukuru na kupongezana kwa bendi hiyo kutwaa tuzo za Kili ikiwemo ile kubwa ya bendi bora ya muziki wa dansi.
Chaz Baba, Jado FFU, Ferguson, Pasyaa na Ferguson wakatengeneza safi ya hatari ya 'ushambuliaji' huku mpiga kinanda Fredy Mazaka, mpiga tumba Dulla Ngoma, mpiga drum Sele Kadance na mpiga solo Amos Nabii na wapiga vyombo wengine wakiujaza muziki mnene na kuufanya ukumbi urindime kwa burudani ya aina yake.
Ni moja ya show ambayo Mashujaa walijitahidi kuitendea haki kila idara kuanzia wacheza show, waimbaji hadi wapiga vyombo. Hadi onyesho linamalizika saa 9.27 za usiku kila mtu alikuwa amezuuzika na roho yake.
Unaweza kusema sentesi moja tu – Mashujaa mwisho wa ubishi.
Comments
Post a Comment