Mashindano ya Mchezo wa Gofu yafanyika jijini Dar



Mashindano ya Mchezo wa Gofu yafanyika jijini Dar
WACHEZAJI 14 kati ya 52 wa mchezo wa gofu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambao mwishoni mwa wiki walishiriki mashindano ya mchezo huo yaliyojulikana kama 'Siku ya Gofu', waliibuka kidedea baada ya kufanya vizuri katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na BancABC.

Mashindano hayo ambayo yalidhaminiwa na BancABC, yalifanyikia kwenye viwanja wa TPDF Lugalo jijini Dar es Salaam. Wachezaji hao ambao walizawadiwa vifaa mbalimbali vya kuchezea mchezo huo ni Peter Fiwa, Moses Namuhisa, Shaban Kibuna, Japhet Masai, Mohabe.

Nyirabu, Joseph Tango, Hitesh Valambia na Gabriel Abel, Olimpia Flaten, F.Gwebe, A.Khamis, Rotsh, S.Denis na g.Kasiga. Akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi,mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo, Boniface Nyoni alisema wameamua kudhamini mashindano hayo kutokana na kuwa wadau wakubwa wa michezo nchini.

Nyoni alisema udhamini wao wa mashindano hayo kwa mwaka huu si mwanzo bali wataendelea kuyadhamini kila mwaka ili kuweza kuuendeleza mchezo huo nchini.

Alisema udhamini wao si kwenye mchezo wa gofu pekee bali ni katika michezo mbalimbali ikiwemo na soka. Naye mmoja wa wachezaji walioshiriki mashindano hayo, George Nyakundi aliipongeza benki hiyo kwa kuamua kudhamini mashindano hayo na kuomba udhamini huo kutoishia mwaka huu.

"Kwa kweli sisi wachezaji wa mchezo wa gofu hatuna budi kupongeza udhamini huu,hivyo na benki nyinge pamoaja na makampuni mengine yaige mfano huu,"alisema Nyakundi.
Mchezaji wa Golf wa Klabu ya TPDF Lugalo, Foti Gwebe akicheza wakati wa mashindano ya mchezo huo ulioshirikisha wateja wa BancABC na baadhi ya wachezaji wa Lugalo Klabu yaliyofanyika Dar es Salam jana.
Mchezaji wa Golf wa Klabu ya TPDF Lugalo, Ally Mfuruki Gwede akicheza wakati wa mashindano ya mchezo huo ulioshirikisha wateja wa BancABC na baadhi ya wachezaji wa Lugalo Klabu yaliyofanyika Dar es Salam jana.
Mchezaji wa Golf wa Klabu ya TPDF Lugalo, Terence Mwakaliku akicheza wakati wa mashindano ya mchezo huo ulioshirikisha wateja wa BancABC na baadhi ya wachezaji wa Lugalo Klabu yaliyofanyika Dar es Salam jana.
Mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya TPDF Lugalo, Brigadia General, Ernest Galinoma akicheza wakati wa mashindano ya mchezo huo ulioshirikisha wateja wa BancABC na baadhi ya wachezaji wa Lugalo Klabu yaliyofanyika Dar es Salam jana.
Mchezaji wa Golf wa Klabu ya TPDF Lugalo, Amina Hamis akicheza wakati wa mashindano ya mchezo huo ulioshirikisha wateja wa BancABC na baadhi ya wachezaji wa Lugalo Klabu yaliyofanyika Dar es Salam jana.


Comments