MANCHESTER UNITED YAJIANDAA KULIPA PAUNI MIL 24 KUMNASA SENTAHAFU WA ATLETICO MADRID

MANCHESTER UNITED YAJIANDAA KULIPA PAUNI MIL 24 KUMNASA SENTAHAFU WA ATLETICO MADRID
MANCHESTER UNITED YAJIANDAA KULIPA PAUNI MIL 24 KUMNASA            SENTAHAFU WA ATLETICO MADRID

MANCHESTER United inatajwa kuwa inakaribia kumalizana na Atletico Madrid ili kumnasa beki wake wa kati Miranda kwa pauni milioni 24.

Miranda, 29 alikuwa na kiwango kizuri msimu ulioisha akiunda ukuta wa mawe kati yake na Diego Godin na kupelekea kikosi hicho cha Diego Simeone kutwaa ubingwa wa La Liga.

Lakini sasa Miranda anataka kusaka changamoto sehemu nyingine wakati Manchester United ikiwa tayari kulipa pauni milioni 24 ili kufikia kipengele cha manunuzi kilichoko kwenye mkataba wake.

Manchester United ipo tayari  kumpa beki huyo ofa ya mktaba wa miaka minne.

Inadaiwa kuwa beki huyo wa Brazil ambaye hayupo kwenye kikosi kitakachocheza kombe la dunia, alikuwa jijini Manchester kuandaa mazingira ya uhamisho wake.

Comments