BAADA ya kazi yake safi ya kuisuka Liverpool, kocha BRENDEN Rodgers amezawadiwa mkataba mpya utakaomuweka Anfield kwa muda mrefu.
Rodgers alikuwa amebakiza miezi 12 kwenye mkataba wake huku kwenye makubaliano yake kukiwa na nafasi ya kuongeza mwaka mmoja.
Lakini badala yake, kocha huyo amesaini mkatabba mpya utakamalizika 2018.
Brenden akasema: "Nina furaha sana kupata nafasi ya kuendelea kujenga msingi tulioanza kuijenga miaka miwili iliyopita na sasa tunakwenda hatua nyingine."
Rekodi ya Rodgers katika Liverpool: Michezo 97 Ameshinda 54 Sare 21 Kupoteza 22
Magoli ya kufunga 206 Magoli ya kufungwa 118
Wastani wa ushindi 55.67
Comments
Post a Comment