LADY JAY DEE KUNG’ARISHA TAMASHA LA WATOTO ‘EXTREME KIDS FESTIVAL’ MAY 31 NA JUNE 1, UWANJA WA LEADERS CLUB


LADY JAY DEE KUNG'ARISHA TAMASHA LA WATOTO 'EXTREME KIDS FESTIVAL' MAY 31 NA JUNE 1, UWANJA WA LEADERS CLUB








Tamasha kubwa la watoto 'Extreme Kids Festival' litakalofanyika May 31 na June 1 katika viwanja vya Leaders Club, Dar es Salaam na litapambwa na mwimbaji mkongwe wa kike anaependwa sana, Lady Jay Dee.
Lady Jay Dee atajumuika na watoto watakaohudhuria tamasha hilo, atawaongoza kuimba nyimbo mbalimbali ili kuwahamasisha kuonesha vipaji vyao na atawapa zawadi wale watakaofanya vizuri zaidi.
"Watoto Mambo vipi, Jay Dee nawakaribisha watoto wote pamoja na wazazi na walezi. Mje basi katika Extreme Kids Festival. Ni Jumamosi ya tarehe 31 May, si hapo tu na Jumapili ya tarehe 1 June. Tunatoa nafasi kwa watoto kuzindua vipaji vyao vya kuimba na washindi watapata zawadi." Amesema Lady Jay Dee kwenye maelezo yake.
Katika tamasha hilo, mbali na michezo/games mbalimbali inayopendwa zaidi na watoto pia kutakuwa na semina fupi kwa ajili ya wazazi na walezi kwa ajili ya kuboresha malezi ya watoto.
Kutakuwa pia na bidhaa mbalimbali huduma muhimu bora zaidi kwa ajili ya watoto na wanafamilia zitatolewa kwa siku hizo mbili.
Waandaaji wa Extreme Kids Festival wamesisitiza kuwa kutakuwa na usalama wa kutosha kwa ajili ya watoto na wote watakaohudhuria na kwamba hakutakuwa na pombe .
Watoto watalipa shilingi 3,000 tu na wakubwa watalipa shilingi 5, 000 tu kuingia katika tamasha hilo.


Comments