Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
MATAIFA mbalimbali barani Afrika leo yanashuka dimbani kusaka nafasi ya kupangwa katika hatua ya makundi kuwania kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika, AFCON 2015 nchini Morocco.
Jana mechi mbili zilipigwa ambapo Kenya walilazimisha sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Comoros na kufanikiwa kusonga mbele kutokana na ushindi wa bao 1-0 walioupata mjini Nairobi.
Sudan kusini waliofungwa mabao 5-0 na Msumbiji mjini Maputo, jana waliwakaribisha wapinzani wao nyumbani na kutoka suluhu ya bila kufungana.
Kwa matokeo hayo, Msumbiji wamesonga mbele na wanasubiri mshindi wa mechi ya Taifa stars na Zimbabwe ili kuumana naye katika hatua ya mwisho kuwania kupangwa hatua ya makundi.
Mechi nyingine zinatarajia kuendelea leo katika nchi mbalimbali barani Afrika.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com
Comments
Post a Comment