KIZUNGA WA TWANGA HALI TETE …alazwa Mwananyamala Hospital



KIZUNGA WA TWANGA HALI TETE …alazwa Mwananyamala Hospital
KIZUNGA WA TWANGA HALI TETE …alazwa Mwananyamala            Hospital

MWANAMUZIKI wa Twanga Pepeta Ismail Kizunga ambaye kwa zaidi ya miaka miwili hayupo jukwaani kwa ugonjwa wa kupooza, amelazwa Hospitali ya Mwananyamala baada ya hali yake kubadilika ghafla.

Kizunga alipelekwa hospitalini hapo mapema leo huku akiwa hawezi hata kuongea.

Meneja wa Aset, Hassan Rehani ameithibitishia Saluti5 kuwa hali ya  Kizunga si nzuri.

"Tulipigiwa simu majira ya saa 5 kuwa hali ya Kizunga ni mbaya, tukaenda nyumbani kwake kumchukua na kumpeleka hospitali," alisema Rehani na kuongeza kuwa mwanamuziki huyo bingwa wa magitaa ya solo na rhythm amelazwa wodi namba tano B.



Comments