KHALID CHOKORAA AINGIA BOXING KWA MGUU WA KULIA, ASHINDA PAMBANO LAKE LA KWANZA



KHALID CHOKORAA AINGIA BOXING KWA MGUU WA KULIA, ASHINDA PAMBANO LAKE LA KWANZA
KHALID CHOKORAA AINGIA BOXING KWA MGUU WA KULIA, ASHINDA            PAMBANO LAKE LA KWANZA

MWIMBAJI na mkurugenzi wa Mapacha Watatu Khalid Chokoraa ameingia vizuri katika masumbwi ya kulipwa baada ya Jumamosi iliyopita kushinda pambano la kwanza.

Chokoraa alijitosa kwenye ukumbi wa Friends Corner Manzese kupambana na Abdul Manyeze na kumshinda kwa 'knock out' ya raundi ya kwanza tu.

Lilikuwa pambano la raundi 4 uzito wa kilo 60, likiwa moja ya mapambano ya utangulizi ya pambano kuu kati ya Said Mbelwe na Karama Nyilawila.

Chokoraa (katikati) akipongezwa baada ya kuibuka mshindi

Tangu sekunde ya mwanzo, Chokoraa alimbana vizuri mpinzani wake ambaye kihistoria, ameshacheza mechi 6.

Chokoraa ameiambia Saluti5 kuwa huo ni mwanzo tu na sasa mapambano mengi yatafuata lakini akaweka wazi kuwa bado anaendelea na muziki.

 

Chokoraa (kushoto) siku ya kupima uzito. Picha zote kwa hisani ya Super D



Comments