KALUNDE BAND TISHA SANA …wapiga bonge la show kuwasindikiza Mashujaa Band Letasi Lounge …pata picha kibaoooo!
KUNA bendi hazina makuu wala kelele lakini ukikutana nao jukwaani utazima zako. Mojawapo ni Kalunde Band.
Kalunde wamepiga bonge la show katika onyesho maalum la Mashujaa Band hapa Letasi Longe, Victoria Jijini Dar es Salaam.
Ni onyesho la kupongezana kwa ushindi wa tuzo tatu za Kili Music Awards ambapo Kalunde wamekuja kama wasindikizaji.
Jamaa wanapiga mziki wa dunia yote, ukitaka copy za kila kona utakoma, ukiskia nyimbo zao wenyewe utapigwa na butwaa. Ni bendi ya watu wachache yenye watu wasiozidi 16 lakini wanashambulia kama mchwa.
Moja ya zawadi nzuri ya Kalunde Band kwenye onyesho hili ilikuwa ni pale walipopiga wimbo Solemba ulioimbwa na Msondo Ngoma miaka ya 80 utunzi wake marehemu Nico Zengekala. Kalunde Waliutendea haki sana wimbo huu ilikuwa ni kama vile Zengekala karejea duniani.
Utawapenda pia walivyo nadhifu jukwaani. Ni aina ya bendi ambayo hutachoka kuitazama.
Kalunde wameshuka jukwaani na kuwapisha Mashujaa Band ambao nao wamepanda na moto mkali. Kama ndo kwanza uko njiani bado hujachelewa.
Comments
Post a Comment