DAVID Luiz wa Chelsea ameuzwa rasmi kwenda Paris St Germain ya Ufaransa kwa dau la pauni milioni 50.
Mchezaji huyo tayari amefuzu vipimo vya afya pamoja na makubaliano binafsi na hivyo kuanzia sasa ni mchezaji halali wa PSG.
Chelsea imethibitisha kupitia website yake kwa kusema: "'Chelsea Football Club na Paris Saint-Germain zimefikia muafaka katika usajili wa David Luiz kwenda timu hiyo ya Ufaransa."
David Luiz mwenye umri wa miaka 27 sasa anakuwa beki ghali duniani akivunja rekodi ya Mbrazil mwenzake Thiago Silva na Marquinhos walionunuliwa na PSG kwa bei mbaya.
Comments
Post a Comment