CHELSEA YAFANYA USAJILI WA KUSHANGAZA, YAMSAJILI TIAGO WA ATLETICO MADRID


CHELSEA YAFANYA USAJILI WA KUSHANGAZA, YAMSAJILI TIAGO WA ATLETICO MADRID

Moving on: Atletico Madrid midfielder Tiago is set to                leave the club on a free transfer next month

CHELSEA imekubali dili la kushangaza la kumrudisha kundini kiungo wa Kireno Tiago aliyepata kuichezea timu hiyo msimu wa 2004 – 05.

Tiago mwenye umri wa miaka 33 aling'ara na Atletico Madrid msimu ulioisha kwa kuchangia kuipa ubingwa wa Hispania pamoja na kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa, lakini sasa yuko huru baada kutopewa mkataba mpya.

Jose Mourinho tayari ametenga pauni milioni 38 ili kumnasa Diego Costa na inaamika kuwa uwepo wa Tiago utamsaidia Costa kupata wepesi wa kuzoea maisha ya Chelsea.



Comments